
![]() |
| Bastola hiyo ilitengenezwa Ubelgiji |
Miaka minne iliyopita, waasi nchini Libya walisherehekea kifo cha aliyekuwa rais Muammar Gaddafi.
Bastola
yake iliyofunikwa imepambwa kwa dhahabu iliinuliwa juu na wapiganaji
hao, ikiwa ishara ya ushindi dhidi ya utawala wa Gaddafi.
Kwa furaha, wapiganaji hao waliipokezana kwa zamu!
![]() |
| Gaddafi aliuawa tarehe 20 Oktoba 2011 |
Bastola hiyo ilikuwa silaha binafsi ya Gaddafi, japo kwa wakati huo
ilibadilika na kuwa ishara ya ushindi kwa waasi, na uhamisho wa mamlaka,
katika mwamko mpya wa Libya.
Mjini Misrata, kilomita 200 mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli, ndipo inapoaminika kuwa bunduki hiyo ipo kwa sasa.
Mwandishi wa BBC Gabriel Gatehouse alishuhudia sherehe hizo zilizohusisha bastola hiyo moja kwa moja.
Na
baada ya miaka minne, Gabriel Gatehouse, amerejea Libya kutafuta
bastola hiyo na pia kuona jinsi maisha yalivyo kwa waasi waliomwangamiza
Gaddafi.
Anaanza kwa kumtembelea mdokezi wake wa zamani Anwar Suwan.
![]() |
| Gabriel Gatehouse akiwa na Anwar Suwan mwaka 2011 |
Alihusika sana katika mapinduzi Misrata. Gaddafi alipouawa,
wapiganaji walipeleka mwili wake kwa Anwar, na Anwar akauweka mwili huo
hadharani watu wauone, ukiwa umewekwa kwenye jokofu kubwa la kuhifadhia
nyama.
Anapomwambia kwamba anamtafuta mtu aliye na bunduki ya
Gaddafi, mara moja anamfikiria Omran Shabaan, mmoja wa wapiganaji
waliomkamata Gaddafi.
Kwenye kanda ya video iliyopigwa na waasi kwa kutumia simu, Shabaan anasikika akiwasihi watu wasimuue Gaddafi.
Mwingine
aliyekuwepo siku hiyo, Ayman Almani, anamwonyesha Gatehouse video
aliyoichukua siku hiyo, ambayo haijawahi kuonyeshwa kwenye vyombo vya
habari awali.
Inaonyesha nyakati za mwisho za kiongozi huyo wa kiimla, anaonekana akitokwa na damu na kuwasihi watu wasimuue.
Omran
Shabaan aligeuka na kuwa shujaa. Alipigwa picha akiwa na video hiyo
iliyopambwa kwa dhahabu na akawa ishara ya matumaini kwamba Libya
ingejikwamua.
Lakini hili halikuwa na mapigano yameendelea.
Mwaka 2012,
Shabaan mwenyewe alikamatwa na wafuasi wa Gaddafi eneo la Bani Walid.
Walimpiga na kumtesa. Wapiganaji wa Misrata walipofanikiwa kumkomboa,
walikuwa wamechelewa sana. Alifariki kutokana na majeraha akitibiwa
hospitali moja Ufaransa.
Anwar Suwan anamwambia Gatehouse kwamba huenda Shabaan alikuwa na bastola hiyo alipokamatwa na wafuasi wa Gaddafi.
Huenda imo mikononi mwa wafuasi hao wa Gaddafi.
Kwenye simu yake ya rununu, Gatehouse ana picha aliyoipiga tarehe 20 Oktoba mwaka 2011 siku ambayo Gaddafi aliuawa.
Ninamuonyesha
picha hiyo. Ni picha ya kijana mmoja, akiwa amevalia shati la rangi ya
samawati, na kofia ambayo ni maarufu na wachezaji wa mpira wa magongo wa
New York Yankees.
“Mohammed Elbibi,” mtu mmoja anamtambua.
Kwenye picha, Mohammed anaonekana akitabasamu huku akibebwa juu kwa juu na wenzake, akiwa ameinua bastola hiyo.
Anwar anasema hajui yaliyomsibu Mohammed lakini anaahidi kusaidia kumtafuta.
Baada
ya muda mrefu, Gabriel Gatehouse, alipata anwani yake Mohammed Elbibi,
kijana aliyekuwa kwenye picha aliyoipiga akiwa ameinua bastola hiyo.
Alimpigia simu na akakubali kukutana naye.
Anapomwonyesha picha yake, anatabasamu na kusema, "naikumbuka, nilikuwa na umri wa miaka 17 wakati huo".
"Bunduki unayo?" Gabriel anauliza.
Mohammed angali anaihifadhi bastola hiyo!
Ni bastola ya milimita 9 aina ya Browning, iliyofunikwa kwa safu nyembamba ya dhahabu ikiwa imepambwa kwa miundo ya maua.
Mohammed anasema kamwe hakumuua Gaddafi.
Anasema
aliokota bunduki hiyo karibu na mahali ambapo Gaddafi alikamatwa, na
katika mtafaruku uliokuwepo, na pia alipoonekana na bastola hiyo, waasi
wengine walidhani Mohammed ndiye aliyemuua Gaddafi, na papo hapo akakuwa
shujaa wa mapinduzi nchini Libya!
Hata hivyo Mohammed anaishi kwa woga.
Wafuasi wa Gaddafi wanatishia maisha yake.
"Tafadhali elezea ulimwengu kuwa sio mimi niliyemuua Gaddafi," Mohammed anasema.
![]() |
| Gatehouse mwishowe alifanikiwa kuiona bastola hiyo |





weka maoni yako (h)
ReplyDelete