
![]() |
Mimba za mapema nchini Thailand |
Thailand imezindua kampeni kabla ya
siku ya wapendanao ya Valentine ikiwataka vijana kutosikia aibu
wanapobeba mipira ya kondumu.
Mpango huo unaonekana kubadilika
ikilinganishwa na kampeni zilizokuwa zikifanywa hapo awali,ambapo vijana
walihamasishwa kuzuru maeneo ya kidini na baadaye kwenda nyumbani baada
ya mikutano na wapenzi wao badala ya kushiriki katika ngono.
Thailand
ina idadi kubwa ya wasichana waliotungwa mimba duniani pamoja na na
viwango vya juu vya magonjwa yanayoambukizwa kupitia ngono.
![]() |
Kampeni ya utumizi wa mipira ya Kondomu nchini Thailand |
Kampeni hiyo inayotarajiwa kuendelea hadi mwaka 2019,inaambatana na
mipiango ya hivi karibuni inayolenga kuangazia mimba za vijana.
Mamlaka zimehamasisha umuhimu wa kutumia mipiria ya kondomu katika miaka ya nyuma pamoja na kuwashuri vijana kutoshiriki ngono.
Lakini
mwaka huu wamesema watalenga kupunguza unyanyapaa kuhusu utumizi wa
kondomu pamoja na kurahisisha upatikanaji wake mbali na kuimarisha
mipira hiyo.
Msemaji wa Wizara ya afya nchini Thailand
Lertwilairrattanapong amesema kwamba vijana hawafai kuaibishwa kuhusu
ununuzi wa mipira ya kondomu.
''Jamii pia inafaa kukubali kwamba
vijana wasichana wanafaa kununua kondomu,ambazo ni bora badala ya
wasichana hao kupata mimba'',Reuters ilimnukuu akisema.
Reviews:
Post a Comment