
![]()
| ||||
Kisa nadra sana cha virusi vya Zika kuambukizwa kupitia kushiriki ngono, badala ya kuumwa na mbu, kimeripotiwa nchini Marekani.
Mgonjwa
aliyeambukizwa virusi hivyo Dallas, Texas, sana huenda aliambukizwa
kupitia kufanya mapenzi, Kituo cha Udhibiti wa Maradhi (CDC) kimeambia
BBC.Mtu huyo hakuwa amesafiri maeneo ambayo yana virusi hivyo lakini mpenzi wake alirejea majuzi kutoka Venezuela.
Virusi vya Zika vinaenezwa sana na mbu na vimehusishwa na visa vya watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo na ubongo kudumaa.
Vinaenea kwa kazi Amerika na Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza hali ya tahadhari duniani.
![]() |
Virusi vya Zika vinaaminika kuwafanya watoto wazaliwe na vichwa vidogo |
Shirika la msalaba mwekundu nchini Marekani limewahimisha watu waliotoka maeneo yaliyoathirika na Zika, na ambao wanataka kutoa damu, wasubiri angalau siku 28, kabla ya kutoa damu.
Ushauri huu umeelekezwa kwa watu waliorejea Marekani kutoka Mexico, visiwa vya Caribbean au Amerika ya Kati na Kusini katika kipindi cha wiki nne zilizopita, shirika hilo limesema kupitia taarifa.
Katika tukio jingine, visa viwili vya maambukizi ya Zika vimethibitishwa Australia.
Maafisa wanasema wakazi wawili wa Sydey waliopatikana na virusi hivyo walirejea kutoka Caribbean majuzi.
Kisa hicho cha maambukizi ya Zika Dllas, kitakuwa ndicho cha kwanza kuthibitishwa kutokea Marekani bara, ingawa jimbo la Texas limeripoti visa vingine ssaba, vyote kwenye watu waliorejea kutoka nje.
Anne Schuchat, naibu mkurugenzi mkuu wa CDC amesema hicho ndicho kisa cha kwanza kinachohusisha mtu ambaye hakusafiri.
Reviews:
Post a Comment