14:20 Tume
ya uchaguzi imetoa matangazo mengine na kufikisha idadi ya vituo
ambavyo matokeo yametangazwa hadi 24,342 (86.9%) kati ya 28,010. Rais
Yoweri Museveni ana kura 5,288,074 (61.88%) naye Dkt Kizza Besigye kura
2,920,664 (34.18%). Tume inatarajiwa kutangaza mshindi kufikia saa kumi
alasiri.
13:47 Gazeti la Daily Monitor linaripoti
kuwa rais wa FDC Mugisha Muntu na Erias Lukwago wa chama cha DP
wamefika nyumbani kwa Dkt Kizza Besigye eneo la Kasangati lakini
wakazuiwa kuingia na maafisa wa usalama waliozingira nyumba hiyo.
13:34 Mwangalizi
mkuu wa Jumuiya ya Madola Olusegun Obasanjo amekosoa baadhi ya mambo
yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu Uganda. Amesema haikuwa haki
kumkamata na kumzuilia Dkt Kizza Besigye.
12:57 Mwangalizi
mkuu wa Umoja wa Ulaya Eduard Kukan amesema hakuna ushahidi wa
kuonyesha kwamba Tume ya Uchaguzi Uganda ilijifunza kutokana na
yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu 2011.
15:57 Mwangalizi mkuu wa Bunge la Ulaya Bw Leinen amesema kuna hatua nyingi ambazo zinafaa kuchukuliwa kuboresha uchaguzi Uganda.
12:04 Mwangalizi
mkuu wa Bunge la Ulaya Jo Leinen asema kulikuwa na kasoro nyingi. Asema
mfano fedha za serikali na chama lazima zitenganishwe. Asema hakukuwa
na usawa katika kuwapa wagombea nafasi katika vyombo vya habari vya
dola. Asema tume pia haikuwapasha raia habari vyema.
11:57 Waangalizi
wa Umoja wa Ulaya: Tutatoa ripoti kamili baadaye ambayo pia itakuwa na
mapendekezo ya hatua zinazofaa kuchukuliwa kuboresha mfumo wa uchaguzi
Uganda.
11:56 Waangalizi wa
Umoja wa Ulaya: Hatua ya kufunga usajili wa wapiga kura Mei 11
uliwafungia watu waliotimiza umri wa miaka 18 baada ya tarehe hiyo.
11:54 Hakuna
mfumo wa kisheria wa kuhakikisha usawa wakati wa kampeni. Sheria za
kufichua fedha za kampeni hazifuatwi na hazitekelezwi.
11:53 Waangalizi
wa Umoja wa Ulaya: Visa vya kukamatwa na kuhangaishwa kwa wapinzani
viliripotiwa katika zaidi ya wilaya 20. Sana waathiriwa walikuwa wa
chama cha FDC.
11:52 Waangalizi
wa Umoja wa Ulaya : "Tume inakosa uwazi na wadau hawana imani nayo. Tume
haina uwazi katika kufanya maamuzi na katika kuwafahamisha wapiga kura
kwa wakati na kwa ufasaha."
11:50 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya washutumu kukamatwa kwa mgombea urais wa chama cha FDC Dkt Kizza Besigye jana.
11:41 Matokeo
ya uchaguzi wa urais ya karibuni zaidi: Vituo 23,308 kati ya jumla ya
vituo 28,010, Rais Yoweri Museveni ana kura 5,047,754 (61.55%) naye
Kizza Besigye 2,826,444 (34.47%). Vituo ambavyo matokeo yametangazwa ni
asilimia 83.21 ya vituo vyote
Reviews:
Post a Comment