![]() |
Bi Congcong alisomea shule ya wasichana ya Feza |
Msichana kutoka China ameibuka wa pili kwa ubora katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta).
Congcong Wang, 16, alifanyia mtihani wake shule ya upili ya wasichana ya Feza iliyoko eneo la Kinondoni, Dar es Salaam.Bi Congcong, aliyepata alama B katika Kiswahili, anatoka jiji la Changchun katika mkoa wa Jilin nchini Uchina.
Ameambia wanahabari kwamba ameshangazwa sana na matokeo hayo.
![]() |
Congcong Wang (kushoto) akiwa na mamake |
"Sijawahi kudhani ningekuwa mmoja wa wanaoongoza. Nimekuwa nikitia bidii masomoni lakini sikutarajia hili,” amenukuliwa na gazeti la The Citizen.
Alijiunga na shule za Feza mwaka 2006 akitokea China na akalazimika kujifunza Kiswahili na Kiingereza.
![]() |
Bi Congcong alipata B katika somo la Kiswahili |
Jumla ya wanafunzi 240,996 walifanya mtihani huo wa kitaifa Novemba mwaka jana
Reviews:
Post a Comment