![]() |
Watts hutoa hewa yake maeneo ya mashambani Uingereza |
Maeneo mengi ya Uchina, hasa miji
mikubwa, yamekuwa yakitatizwa na uchafuzi wa hewa. Hili limekuwa faraja
kwa Mwingereza mmoja ambaye ameanza kuuza hewa safi huko.
Leo De
Watts, 27, hutoa hewa yake maeneo ya mashambani Uingereza ambayo
hayajachafuliwa, kuipakia kwenye chupa na kuisafirisha hadi miji ya
Shanghai na Beijing.
Huko huwauzia matajiri hewa hiyo.
Chupa moja ya hewa safi ya mililita 580 huwa anauza £80 ($115).
Ameanzisha kampuni kwa jina Aethaer na hutoa hewa yake maeneo yenye upepo mwingi ya Dorset, Somerset, na Wales.
Anasema
baadhi ya wateja hutaka hewa ya kiwango fulani na wakati mwingine
humbidi kutoa hewa maeneo ya milima, na wakati mwingine bondeni ili
kupata aina ya hewa inayohitajika na wateja.
"Linaonekana kama
wazo la kushangaza sana kwetu hapa Uingereza kwa sababu tuna hewa safi.
Hapa mtu anayeishi karibu na ziwa akianza kupakia hewa safi kwenye
mikebe na kuuza, marafiki zake watadhani amerukwa na akili,” alisema Bw
Watts alipohojiwa na Stephen Nolan wa BBC 5 Live. ![]() |
Viwango vya uchaguzi wa hewa Uchina vilizidi Desemba |
“Lakini huko hakuna hewa safi na inathaminiwa sana.”
Viwango vya uchafuzi wa hewa Uchina vilifikia viwango vya juu sana hasa mwezi Desemba, na katika baadhi ya maeneo kusababisha shule kufungwa.
- Ukungu: Agizo la kutotoka nje China
- Ukungu: China yatoa ilani karakana zifungwe
![]() |
Hapa Li Tianqin anaonekana akimpa hewa safi bintiye wa umri wa miaka 3 Beijing Desemba mwaka jana |
Li Tianqin ni mmoja wa walionunua mkebe wa hewa safi kutoka Rocky Mountains, nchini Canada.
Kampuni ya Vitality Air, inayovuna hewa hiyo Rocky Mountains, imekuwa ikiuza mkebe mmoja wa hewa kwa kati ya $14 na $20.
Reviews:
Post a Comment