![]() |
Wanawake wenye mapigo ya moyo yanayobadilika wamo katika hatari ya kufa ama kupata kiharusi. |
Mabadiliko ya mapigo ya moyo ni ya
hatari kwa wanawake zaidi kuliko wanaume, kwa mujibu wa tafiti 30 ,
zilizohusisha zaidi ya wagonjwa milioni nne.
Kwa mujibu wa utafiti
huo wanawake wenye mapigo ya moyo yanayobadilika badilika (AF) walikuwa
na uwezekano wa kufa kwa maradhi ya moyo ama kiharusi mara mbili zaidi.
Wanawake
mara nyingi hawaponi vizuri kwa dawa za kudhibiti mabadiliko ya mapigo
ya moyo ama hupatikana na maradhi ya moyo baadae kuliko wanaume.
"Uwezekano
mmoja ni kwamba wanawake wenye mapigo ya moyo yanayobadilika hawatibiwi
ipasavyo ikilinganishwa na wanaume ," Connor Emdin na wenzake ,katika
chuo kikuu cha Oxford, walieleza.
Wakati huo huo, wataalam wanasema madaktari hawanabudi kuelewa kuhusu uchunguzi huu ili kuepuka vifo vinavyoweza kuzuiwa.
![]() |
Takrban watu milioni moja wanatatizo la mabadiliko ya mapigo ya moyo nchini Uingereza |
Takriban watu milioni moja nchini Uingereza wana mapigo ya moyo yanayobadilika.
Unaweza kujichunguza mwenyewe ikiwa una tatizo hilo kwa kuhisi mapigo yako kwa sekunda 30.
Ni
jambo la kawaida kuhisi mabadiliko ya mapigo ya moyo mara chache ,
mfano kukosa kwa pigo moja, kukosa kwa pigo moja ama mapigo zaidi, ni
jambo la kawaida si jambo la kukutia hofu .
![]() |
Mapigo ya moyo ya kazi kubwa yanaweza kusababisha uchovu na kupungua kwa pumzi |
Lakini ikiwa ikiwa utahisi mapigo ya moyo yatabadilika kwa kipindi kirefu , unapaswa kumuona daktari.
Mapigo
pia yanaweza kuwa ya kasi sana , zaidi ya mapigo 100 kwa dakika
unapokua umetulia husababisha uchovu na kupungua kwa pumzi.
Dawa zinaweza kudhibiti hali hii na kuzuia hatari ya kiharusi (kuganda kwa damu ama kuvuja kwa damu kwenye ubongo).
Reviews:
Post a Comment