Madaktari wa Australia wamefanikiwa
![]() |
Mashine iliyotumika kuuhisha moyo uliokufa na kisha kupandikiza kwa mgonjwa |
kuwarejeshea uhai wagonjwa watatu
baada ya kupandikizwa moyo uliokufa
katika operesheni ya kwanza kufanyika
duniani.
Madaktari katika
hospitali ya St Vincent
mjini Sydney walitumia dawa ya kuzuia
kuharibika
iliyotengenezwa na Taasisi ya
Utafiti wa Moyo ya Victor Chang kwa
kupandikiza viungo kwa Michelle Gribilas,mwenye umri wa miaka 57 na Jan
Damen mwenye umri wa miaka 44, huku mgonjwa wa tatu akiendelea kupona.
Moyo
mmoja, ulisimama mapigo kwa dakika 20 kabla ya kuurejesha katika uhai,
ukiwa umewekwa katika mashine na kuuchoma dawa ya kuzuia kuharibika.
![]() |
Jan Damen na mkewe Silvana |
picha na mke wake Silvana) alipandikizwa moyo
uliokufa na kuupa uhai.
Wagonjwa wawili waliopandikizwa moyo (Michelle
Gribilas, kushoto, na Bwana Damen, katikati)
wanazungumza na daktari wa upasuaji
Kumud Dhital
Moyo unahuishwa baada ya kupoteza uhai na
kupandikizwa. Hospitali hiyo inaamini asilimia 30 za watu watarejeshewa uhai kutokana na kugunduliwa kwa dawa hii, ambayo hupunguza kiwango cha uharibifu kwenye moyo na kuwa tayari kupandikizwa.
![]() |
Michelle Gribilas (kushoto) Jan Damen(katikati) wakizungumza na daktari wao Kumud Dhita |
wamekuwa wakitumia moyo kutoka kwa watu
waliokufa kwa asilimia 100 ambao katika uhai
wao walitaka viungo vyao vitumiwe na watu
wengine wenye kuhitaji, lakini sasa upatikanaji
wa moyo utaongezeka zaidi.
Dawa hiyo iliyochukua miaka 12 kuitengeneza,
pia inasaidia kuimarisha kazi ya moyo ambao
unatolewa baada ya kifo (DCD) wakati ukianzishwa
kufanya kazi upya.
Bi Gribilas, ambaye amestaafu na kuishi Campsie kusini magharibi mwa Sydney, amesema ni mtu tofauti kwa sasa baada ya kupandikizwa moyo mpya.
Reviews:
Post a Comment