
Morocco inasema kuwa itawarudisha nyumbani raia wake ambao wameshindwa kupata kibali cha ukimbizi nchini Ujerumani.
Taarifa
kutoka taifa hilo zinasema kuwa mfalme Mohammed alifanya mazungumzo
kupitia njia ya simu na kansela wa Ujerumani Angela Merkel siku ya
Jumatano.Taarifa hiyo imesema kuwa mataifa hayo mawili yalikubaliana kuangazia visa vya wale wanaoishi Ujerumani bila vibali na kwamba watarudishwa nchini Morocco bila kupoteza wakati.
Maelfu ya wahamiaji na wakimbizi kutoka kaskazini mwa Afrika wamejaribu kuingia Ulaya katika siku za hivi karibuni.
Reviews:
Post a Comment