
Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa vibaya katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kufuatia milipuko 3 ya guruneti.
Duru
zinasema kuwa takriban watu wanne wamejeruhiwa baada ya watu
wasiojulikana kutupa gruneti nje ya jumba la posta mjini Bujumbura.
Mlipuko mwengine ulitokea nje ya afisi za kampuni inayotoa huduma za simu nchini humo Lumitel.
Mlipuko wa tatu ulisikika takriban nusu saa baadaye katika soko la zamani.
Hadi tulipochapisha taarifa hii hakuna maelezo kamili hayajatolewa kuhusu nani aliyetekeleza mashambulizi hayo na kwanini.
Machafuko
nchini humo yalitibuka mwezi Aprili mwaka wa 2015 baada ya rais Pierre
Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania uchaguzi katika muhula wake wa tatu.
Wapinzani wake walisema Nkurunziza alikuwa anakiuka katiba ya taifa na kisha maandamano yakaanza kukotokea.
Kulitokea
jaribio la mapinduzi ambayo ilizimwa na kisha rais huyo akaibuka
mshindi katika uchaguzi ambao ulisusiwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa
wa upinzani.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Prime Ndikumagenge, anasema kuwa
mashambulizi haya leo ni ya kipekee kwa sababu ni mara ya kwanza kuwahi
kutokea mchana.
''kumekuwa na mashambulizi mengi nchini ,lakini hii ndio mara ya kwanza kwa mashambulizi ya aina hii kutokea mchana''.
Takriban
watu 439 wameuawa huku wengine 240,000 wakitoroka nchini kuwa wakimbizi
nje ya nchi kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.
Mwezi
uliopita shirika linalopigania haki za kibinadamu Amnesty International
walisema kuwa picha za setlaiti zinaonesha uwezekano wa kuweko kwa
makaburi 5 ya halaiki nje ya Bujumbura.
Maafisa wa usalama wanalaumiwa kwa kuua watu mwezi desemba mwaka uliopita.
Reviews:
Post a Comment