Mahakama moja ya kijeshi nchini Misri
ilimuhukumu kwa makosa kijana mmoja
wa miaka minne kifungo cha maisha jela
kwa mauaji wiki iliopita,jeshi limekiri.
Msemaji wa
jeshi Kanali Mohammed Samir amesema kuwa mahakama hiyo badala yake
ingemshtaki na makosa kama hayo kijana mwenye umri wa miaka 16 mwenye
jina kama hilo.
Ahmed Mansour Qurani Ali alipatikana na hatia
pamoja na wengine 115 kuhusiana na ghasia zilizotekelezwa na wafuasi wa
kundi la Muslim Brotherhood katika jimbo la Fayoum mwaka 2014.
Wakili wake aliwasilisha stakhabadhi akithibitisha alikuwa yeye wakati huo.
katika
chapisho lililowekwa katika mtandao wa facebook kwa lugha ya
kiarabu,Kanali Samir alisema kuwa Ahmed Mansour Qurani Sharar mwenye
umri wa miaka 16 angehukumiwa na wala sio Ahmed Mansour Qurani Ali.
Haijulikani ni nini haswa kitakachompata kijana huyo wa miaka 4.
Wakili
wa mtoto huyo alisema kuwa jina lale liliongezwa katika orodha ya
washukiwa kwa makosa,na kwamba maafisa wa mahakama hawakupeleka kibali
chake cha kuzaliwa kwa jaji ili kuthibitisha umri wake wakati wa kosa
hilo.
Alihukumiwa na mashtaka manne ya mauaji,jaribio la mauji na kuharibu mali ya serikali.
Reviews:
Post a Comment