
Waziri mmoja wa Afrika Kusini ameshtumu kuwa kinyume cha sheria ufadhili wa elimu ya wasichana wanaopita kipimo cha ubikira.
Mwezi
Uliopita,Manispaa ya uthukela katika jimbo la Kwazulu Natal nchini
Afrika Kusini ilisema itawapa zawadi wanafunzi 16 wa kike kwa masharti
kwamba wasalie mabikira.
''Mpango huo ulilenga kupunguza
maambukizi ya virusi vya HIV na mimba za mapema miongoni mwa
wasichana'',alisema Meya Dudu Mazibuko.
Katika taarifa ya gazeti
la Daily Maverick,waziri wa maendeleo ya kijamii Bathabile Dlamini
alielezea upimaji wa ubikira kama usiowezekana,mchafu na ukiukaji mkubwa
na haki za kibiniaadamu.
''Kujamiana kwa mara ya kwanza
hakutakikani,licha ya hilo kuna unyanyapaa miongoni mwa wasichana ambao
hufeli kipimo hicho'',alisema,akiutaja mpango huo kama ''kosa la
kingono''.
Bi. Dlamini ,ambaye ni kiongozi wa chama tawala cha ANC
upande wa wanawake ndio kiongozi mwenye hadhi ya juu kupinga kipimo
hicho.
Reviews:
Post a Comment