
![]() |
Wazee ndio walio na raha zaidi |
Umri wa kati ya miaka 65 na 79 ndio ulio na raha tele miongoni mwa watu wazima ,kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la utafiti wa takwimu za kitaifa nchini Uingereza.
Utafiti
huo uliofanyiwa zaidi ya watu 300,000 nchini Uingereza ulibaini kwamba
kujikimu kimaisha ,furaha na kujihisi unaishi vyema vyote vilipatikana
katika umri huo ,lakini furaha hiyo ikaisha kufikia mwaka wa 80.
Wale
walio na umri kati ya 45 na 59 waliripoti viwango vya chini vya
kujikimu kimaisha, huku wanaume wakijihisi hawafurahi ikilinganishwa na
wanawake.
Umri huo pia uliripoti visa vingi vya kuwa na wasiwasi.wanasayansi wa Navu wameelezea vile furaha hubadilika kulingana na umri.
Utafiti
huo uliwauliza watu kupima kati ya kiwango cha 10, wana raha kwa
kiwango gani na wamekuwa na wasiwasi wa kiwango gani katika siku moja
iliopita,wanahisi vipi kuhusu kujikimu kimaisha na kwa kiwango gani
wanaona kwamba kile walichokitenda kina thamani maishani.
Reviews:
Post a Comment