Operesheni ya ukahaba yanasa wengi Dar es Salaam
Siro
Kamishna Siro amesema biashara hiyo ina uhusiano na uhalifu

Wasichana wapatao 500 wanaodaiwa kufanya biashara ya ukahaba nchini Tanzania pamoja na wateja wao zaidi ya 200 wanashikiliwa na polisi nchini.

Walikamatwa kufuatia msako unaoendelea kukomesha biashara hiyo ambayo haikubaliki kwa mujibu wa sheria nchini humo.
Hii ni idadi kubwa kuwahi kukamatwa katika vita dhidi ya biashara ya ukahaba nchini humo.
Wengi walikamatwa maeneo ya Kinondoni, Temeke na Ilala 51.
Kamishna wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam amesema wengi wa majambazi hukimbilia kwa biashara ya ukahaba.
“Kuwakamata na kuwahoji kunasaidia kupata mambo mengi sana kuhusiana na haya (uhalifu), hata madawa ya kulevya pia. Wengi unakuta wanajua watu wanaoyatumia, wengine wanashiriki,” aliambia wanahabari.
Aliwaomba wananchi kuwasiadia maafisa wa polisi katika operesheni hiyo.

Reviews:

Post a Comment

PRINCE PRODUCT © 2014 - Designed by Templateism.com, Plugins By MyBloggerLab.com | Published By Gooyaabi Templates

Contact us

Powered by Blogger.