![]() |
Mlipuko uliotokea katika msikiti wa Nigeria hapo awali |
Mlipuaji wa kujitoa mhanga amewaua waumini 22 katika msikiti mmoja kando kando ya mji wa Kaskazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria kulingana na chombo cha habari cha AP.
Mlipuaji wa kwanza alijilipua ndani ya msikiti huku wa pili
akijilipua nje huku walionusurika wakijaribu kutoroka walioshuhudia
waliambia BBC.Watu wengine 17 walijeruhiwa katika shambulio hilo afisa
mmoja wa AFP amesema.
Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wamekuwa wakiulenga mji huo katika mashambulio yao ya miaka 17.
''Tulikuwa
mita chache kutoka katika msikiti huo wakati tuliposikia sauti kubwa na
kile kilichofuatia ni moshi mkubwa na mili iliokuwa imetapakaa kila
mahali,shahidi mwengine alikimbia kituo cha habari cha AP.
Shambulo hilo lilifanyika dakika chache tu baada ya waumini kuanza ibada ya alfajiri ,imam mkuu wa Umarari Mosque aliambia BBC.
Wote waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini,aliongezea.
Reviews:
Post a Comment