
Saa za kisasa ambazo zimetengenezwa
mahususi kutumiwa kudanganya wakati wa mtihani zimekuwa zikiwakosesha
usingizi walimu na wasimamizi wa mitihani.
Saa hizo zina uwezo wa kuweka akiba data na maelezo ambayo yanaweza kusomeka mtu anapofanya mtihani.
Aidha,
zina kitufe cha dharura ambacho kinaweza kubadili uso wa saa hizo
haraka sana na badala ya kuonesha habari ziwe zinaonesha uso wa kawaida
wa saa.
Saa hizo zinatangazwa katika soko la kuuza bidhaa mtandaoni la Amazon.
Mojawapo
ya aina ya saa hizo ina uwezo wa kuweka akiba data ya 4GB. Nyingine,
ambayo itaanza kuuzwa baadaye mwaka huu, itakuwa na uwezo wa 8GB na
inaweza kuhifadhi hata video.
Baadhi ya saa hizo, zina kifaa
kidogo sana cha kusikizia ambacho hakitumii nyaya, jambo linalowezesha
mtu kusikiliza kilichohifadhiwa kwenye saa hiyo bila kuonekana.
Tangazo moja katika mtandao wa Amazon linasema mtu anaweza kununua saa ya aina hiyo kwa $61 (£43).
Kuna pia matangazo ya saa hizo eBay.
Naibu
mwalimu mkuu wa shule moja kutoka Bath, Uingereza anasema saa hizo
zinaweza zikawashawishi wanafunzi kuhadaa katika mtihani.
Bw Joe
Sidders wa shule ya Monkton Combe Senior School amesema ingawa saa hizo
zinaweza kudhibitiwa kwa kutumia sheria zinazoharamisha simu na kompyuta
kutoka vyumba vya mitihani, ni changamoto kubwa sana kwa watu
wanaosimamia mitihani.
Amesema uuzaji wa saa hizo unafaa kudhibitiwa.
Kuna pia “kalamu za kuiba mtihani” ambazo zinaweza kuhifadhi habari na maelezo.
Ongezeko la matumizi ya saa kuiba yamefanya baadhi ya mashirika kupiga marufuku saa katika vyumba vya mitihani Uingereza.
Reviews:
Post a Comment