
Watafiti nchini Marekani wametoa
onyo kuwa inaweza kuchukua miongo kadhaa ili kupatikana kwa kinga ya
virusi vya Zika kutengenezwa .Wanasayansi hao wa chuo kikuu cha Texas
kimesema kuwa muda mrefu hadi chanjo hiyo kupata idhini. Wanasema virusi
vya mbu hawa vinaweza kuleta majanga makubwa zaidi.Na suala hili
limehusishwa na madhara ya ubongo wakati mtoto akiwa tumboni.
Hata
hivyo watafiti nchini marekani wamelitaka shirika la afya duniani WHO
kuchukua hatua ili kukabiliana na usambaaji wa virusi vya Zika, ambavyo
vimesemekana kuwa ni athari kubwa.Rais Barack Obama ametaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kupata chanjo na tiba ya ugonjwa huo. msemaji wa Ikulu ya White House, Josh Earnest,amesema kipaumbele cha serikali ya Marekani ni kutoa elimu kwa uma kuhusu athari ya ugonjwa huu. Ernest anasema kwamba: "Tumejikita kwenye ushauri wa kisayansi uliopo ili kuwalinda wamarekani na cha muhimu na kwanza kabisa tumeanza kwa kutoa tahadhari kwa watu kuhusu mipango yao ya kusafiri kwa kuwa wanaweza kwenda eneo ambalo virusi vya ugonjwa huu vipo. Tunataka kuwa na uhakika kuwa watu wanapata elimu ya kutosha kuhusu athari ya virusi hivi lakini pia tunachukua kila hatua ili kutoa tahadhari ambazo ni muhimu kuchukuliwa ili kupambana na ugonjwa huu."
Reviews:
Post a Comment