
Zambia na Mali zimefuzu kwa robo
fainali ya michuano ya kombe la taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa
ligi za ndani baada ya kutoka sare mechi iliyochezwa Jumatano.
Chipolopolo
tayari walikuwa wamefuzu kabla ya mechi hiyo nao Mali walijihakikishia
nafasi ya kufuzu kwa kupata alama hiyo moja kwa kutoka sare tasa
uwanjani Rubavu.Katika mechi nyingine ya Kundi D, Zimbabwe walitoka sare na Uganda, baada ya Cranes kusawazisha dakika ya 93.
William Manondo alikuwa ameweka Zimbabwe kifua mbele lakini Geofrey Serunkuma akasawazisha dakika za mwisho.
Uganda walihitaji kuishinda Zimbabwe nao Mali washindwe na Zambia ndipo wapate nafasi ya kufuzu.
Kwenye Kundi hilo, Zambia walimaliza kileleni na alama 7, Mali wa pili na alama 5, Uganda tatu na alama 2 nao Zimbabwe wakashika mkia na alama 1.
Mechi za robofainali zitachezwa Jumamosi na Jumapili, mechi inayosubiriwa sana ikiwa kati ya wenyeji Rwanda na majirani wao DR Congo Jumamosi uwanjani Amahoro.
Reviews:
Post a Comment