![]() |
Barcelona yaiadhibu Arsenal kwa mabao 2-0 |
Klabu ya soka ya Barcelona imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya klabu bingwa barani ulaya (UEFA) mchezo uliopigwa uwanja wa Emirates . Mabao ya Barcelona katika mchezo huo yamefungwa na mchezaji Lionel Messi dakika ya 71 na Dakika ya 83 likiwa ni bao la pili lililofungwa kwa njia ya penati .
Katika
mchezo mwingine Juventus wakiwa nyumbani dhidi ya Buyern Munich ,mchezo
huo umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kufuatia sare ya
kufungana mabao 2-2.
Buyern Munich ndio walioanza kuzigusa nyavu
za wapinzani kwa kuandika bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wao
Thomas Muller dakika ya 43, muda mchache baadaye Arjen Robben akaandika
bao la pili kwa buyen Munich katika dakika ya 55 kipindi cha pili.
Kwa
upande wao Juventus walizinduka na kuandika bao la kwanza kupitia kwa
Paulo Dybala ikiwa ni dakika ya 63 kipindi cha pili, huku Stefano
Sturaro akiandika bao la pili la kusawazisha dakika ya 76 na kuufanya
mchezo umalizike kwa sare ya kufungana bao 2-2.
Michuano hiyo
itaendelea tena Jumatano kwa Mechi 2 Dynamo Kiev ikiikaribisha Man City
huko Ukraine na PSV Eindhoven wao watakuwa Wenyeji huko Uholanzi dhidi
ya Atletico Madrid.
Reviews:
Post a Comment