![]() |
Meneja Schmidt alikataa kuondoka eneo la kiufundi |
Refarii mmoja nchini Ujerumani alishangaza wengi baada yake kuondoka uwanjani na kuacha mechi imesimama kufuatia kisa kilichomhusisha meneja wa timu moja iliyokuwa ikicheza uwanjani.
Refa Felix Zwayer aliondoka baada ya meneja wa Bayer
Leverkusen Roger Schmidt kukataa kutii amri yake ya kumtaka aondoke
uwanjani kwa kosa la kulalamika sana.
Mechi hiyo ya Bundesliga
dhidi ya Borussia Dortmund ilicheleweshwa kwa dakika nane hivi na
ilirejelewa baada ya Schmidt mwishowe kukubali kuondoka eneo la
kiufundi.
Schmidt alikuwa amedai kuwa bao la Dortmund, lililofungwa na Pierre-Emerick Aubameyang, halikufaa kukubaliwa.
Mkufunzi huyo wa umri wa miaka 48 alisema mkwaju wa adhabu uliopelekea kufungwa kwa bao hilo haukupigiwa eneo sahihi.
![]() |
Zwayer baadaye alirejea baada ya Schmidt kukubali kuondoka |
Kutokana na kulalamika kwake, alifukuwa eneo la kiufundi, lakini akakataa kubanduka.
Refa
Mjerumani Zwayer alimsihi kaimu nahodha wa Leverkusen Stefan
Kiessling, aliyekuwa amefanya madhambi yaliyosababisha mkwaju huo wa
adhabu, amsihi meneja wake aondoke.
Baada ya hilo kushindikana, Zwayer aliondoka uwanjani na kuingia chumba cha kubadilishia mavazi. Alifuatwa na wachezaji.
“Nakubali, nilifanya kosa. Lakini refa angenifafanulia ni kwa sababu gani alikuwa akinifukuza,” Schmidt alijitetea baadaye.
Reviews:
Post a Comment